JE, UNGEPENDA KUMPIGIA MTU SIMU ASIYOJUE SI WEWE ? BASI…
(Kwenye filamu labda, lakini si Tanzania…)
Unawahi kufikiria jinsi inavyokuwa kwenye movie zile kali? Mtu anapiga simu, lakini upande wa pili unaona tu: "Private Number" au "Unknown Caller" — unajikuta unashangaa ni nani huyo, unapokea kwa hofu, au unakataa kabisa.
Basi, pengine nawe umewahi kutamani kujaribu hiyo trick — kuficha namba yako kwa makusudi ili:
Upige bila kujulikana
Ufanye surprise call
PIGA CODE *31#
Lakini dah, kwa bahati mbaya…
Kwa sisi waTanzania, hiyo mbwembwe ya kuficha Caller ID haipo ๐คฃ
Ukiitumia, badala ya kupiga kimafia, simu yako haitapiga kabisa mpaka urudishe Caller ID!
Kwa Nini Hivi Inashindikana Coz nchi yenu inasema nyie ni matapeli wa mtandaoni ๐คฃ
Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeweka masharti maalum yanayowataka mitandao yote (Vodacom, Airtel, Tigo, Halotel n.k.) kuhakikisha kuwa kila simu inayoingia na kutoka inaonyesha namba ya mpigaji. Hii ni kwa sababu:
Kuzuia uhalifu wa kimtandao na vitisho kupitia simu.
Kuwezesha usalama wa kitaifa – serikali iweze kufuatilia mawasiliano yoyote yanayokiuka sheria.
Kufuatilia makosa ya jinai kwa kutumia ushahidi wa mawasiliano.
Kwa hivyo, ku-disable Caller ID (kutumia #31# au kuzima kwa settings) kunaifanya simu yako ishindwe kabisa kupiga mpaka uwashe tena.
Kwa Wanaojaribu Ku-bypass…
Hata ukibadilisha line, simu, au OS — kama uko Tanzania na unatumia line ya Tanzania, system ya mtandao itakataa.
Hii trick inafanya kazi kwa baadhi ya nchi tu, lakini sio kwenye ardhi ya bongo yetu!
Kwa ufupi: Nikijipata tyuuuu nasepa nchini kwenu sitaki ujinga ๐คฃ mna banwa Kila idara ๐คฃ sasa mawasiliano mnafatilia wakati account za police zilihakiwa
> All right reserved by. Ceo Tech and his support team
