Ufafanuzi: VPN vs No VPN
Mchoro huu unafafanua wazi jinsi data yako inavyosafiri kupitia mtandao, na jinsi Virtual Private Network (VPN) inaweza kulinda faragha na usalama wako. Kimsingi, inakuonyesha jinsi data inavyosafiri ikiwa imefichwa na ikiwa wazi.
Kutumia VPN
Sehemu ya juu ya mchoro inaonyesha jinsi VPN inavyofanya kazi. Kifaa chako kwanza huunganishwa na VPN Client, ambayo hutengeneza handaki salama (encrypted tunnel) kwa data yako. Data hii hupelekwa kupitia ISP wako ikiwa imefichwa, hivyo ISP haiwezi kuiona. Baada ya kupita kwa ISP, data huenda kwenye VPN Server, ambapo inafichuliwa kabla ya kupelekwa kwenye Internet. Hii huifanya ISP na wahalifu wa mtandaoni wasiweze kufuatilia shughuli zako.
Kutotumia VPN
Sehemu ya chini inaonyesha mtandao bila VPN. Hapa, kifaa chako huunganishwa moja kwa moja na ISP. Data yote, ikiwemo tovuti unazotembelea na vitu unavyofanya mtandaoni, hupita kwa ISP ikiwa wazi (unencrypted). Hii inaipa ISP uwezo wa kuona na kurekodi shughuli zako zote, na pia inakufanya uwe hatarini zaidi dhidi ya mashambulizi ya mtandaoni.